Wikimania inaadhimisha mwaka wake wa 20 kwa toleo lake la kwanza kabisa katika Afrika Mashariki, na umealikwa kwa moyo mkunjufu! Iwe ana kwa ana au mtandaoni, tungependa ujiunge nasi katika kuadhimisha miaka 20 ya mikusanyiko ya kimataifa ambayo huimarisha jinsi tunavyounda na kushiriki maarifa bila malipo.
Kwa wale wanaopenda kuhudhiria mkutano huo jijini Nairobi, Timu Kuu ya Maandalizi inazindua maombi ya ufadhili mapema mwaka huu. Matumaini yetu ni kufanya mipango ya usafiri, ikiwa ni pamoja na mchakato wa visa, kuwa rahisi iwezekanavyo kwa wafadhiliwa waliokubaliwa.
Tuma ombi la kuhudhuria Wikimania 2025 jijini Nairobi kabla ya tarehe 8 Desemba 2024.
Maelezo ya mkutano
Ikiletwa kwenu na timu ya Wanawikimedia kutoka kote kanda ya Afrika Mashariki, mada ya Wikimania 2025 itakuwa “Wikimania@20: Inclusivity. Impact. Sustainability” ambayo inalenga kusherehekea hatua muhimu na matokeo ya harakati zetu huku ikifungua njia ya majadiliano kuhusu mikakati na mipango inayohakikisha uendelevu wa miradi ya Wikimedia na ujumuishaji katika harakati.
Mkutano utafanyika kutoka tarehe 6-9 Agosti, na shughuli za kabla ya mkutano pia zinapangwa mnamo tarehe 5 Agosti. Maelezo zaidi kuhusu programu na ukumbi yatashirikiwa hivi karibuni.
Maelezo ya maombi
Tunakuhimiza kufanyia kazi ombi lako la ufadhili sasa. Maombi yatathminiwa kulingana na kuhusika kwako na ushiriki katika kukuza uthabiti na uendelevu wa harakati zetu -iwe ni katika shughuli za mtandaoni au nje ya mtandao. Tafadhali hakikisha kuwa umetoa melezo ya michango yako kwa kina hadi sasa kwa harakati za Wikimedia, ukiangazia matokeo ya michango hiyo na kuunga mkono hoja zako kwa viungo inapowezekana. Wanawikimedia kutoka kanda ya Afrika Mashariki, pamoja na Wanawikimedia walio na haki zaidi za utumiaji, wanahimizwa haswa kutuma maombi-tunatumai kuwa na uwezo wa kuwezesha ushiriki wa ujuzi ndani na katika kanda zote kupitia tukio la mwaka huu.
Ufadhili utagharimia usafiri, malazi na usajili. Kama ilivyokuwa miaka iliyopita, wafadhiliwa wataombwa kujitolea kwa saa 4-6 katika kipindi cha Wikimania, wakiwa na chaguo la kujitolea kwa muda zaidi ikihitajika. Wapokeaji wote wa ufadhili watashughulikiwa kwa Sera ya Bima ya Usafiri ya Shirika la Wikimedia Foundation.
Waombaji watajulishwa kuhusu matokeo ya maombi yao mwezi Machi.
Maswali?
Unaweza kusoma zaidi kwenye Wikimania Wiki na kuifikia timu kwa maswali yoyote katika wikimania-scholarships@wikimania.org.
Karibuni Nairobi!
Tazama taarifa ya faragha ya uchunguzi.
Can you help us translate this article?
In order for this article to reach as many people as possible we would like your help. Can you translate this article to get the message out?
Start translation