Tuma maombi sasa ili kuzungumza katika Wikimania 2025

Translate this post

Siku zimeanza rasmi kuhesabika kuelekea Wikimania 2025! Toleo la 20 la Wikimania litaadhimishwa jijini Nairobi, Kenya kuanzia tarehe 06-09 Agosti 2025. Na kwa nini utazame tu wakati unaweza kuwa sehemu ya tukio? La mgambo limelia, wito wa mapendekezo ya programu uko wazi!

Tunatafuta mawasilisho ambayo yanahusiana na mada yetu ya 2025, “Wikimania@20: Ujumuishi. Athari. Uendelevu.” Sasa ni wakati mwafaka wa kuwa na mazungumzo kuhusu:

  • Ujumuishaji: Je, tunaundaje nafasi ambapo kila mtu anahisi kuonekana, kusikilizwa, na kuthaminiwa kushiriki katika jumla ya maarifa yote? Hebu tuzungumze kuhusu njia za kukuza ushiriki tofauti, kuondoa vizuizi, na kuhakikisha ufikiaje kwa wote.
  • Athari: Wacha tusherehekee athari zetu na kule tulikotoka, kwa kutambua hatua muhimu ambazo zimeunda harakati zetu katika miongo miwili iliyopita. Lakini pia tuangalie mbele: Je, tunawezaje kuendeleza kasi hii ili kuleta athari kubwa zaidi katika siku zijazo?
  • Uendelevu: Je, tunahakikishaje kwamba harakati zetu hazidumu tu bali pia zinastawi kwa muda mrefu? Hebu tuzungumze kuhusu kile kinachohitajika ili kuunda athari ya kudumu, kusaidia vizazi vijavyo vya Wanawikimedia, na kuendeleza miradi yetu kwa miaka mingi.

Je, uko tayari kushirikisha maarifa yako na kuwatia moyo wana Wikimedia wenzako? Tuma ombi sasa ili kuongoza warsha, kukaribisha jopo, kuwasilisha bango, au kuonesha onyesho la zana miongoni mwa mengine. Iwapo unapendelea kuzungumza ana kwa ana, mtandaoni, au katika muundo wa mseto, tunakaribisha pendekezo lako. 

Wasilisha kipindi chako mpaka tarehe 31 Machi popote pale duniani 23:59 UTC-12 (angalia saa za eneo lako). Unaweza kufanya hivyo kwa kujaza fomu ya maombi na kujifunza zaidi kuhusu mchakato wa upitiaji wa maombi kwenye Wikimania Wiki. Timu ya kuandaa itawasilisha maamuzi kuhusu mapendekezo mnamo Juni 2025. 

Tazama tamko la ya faragha kuhusu Maombi haya.

Can you help us translate this article?

In order for this article to reach as many people as possible we would like your help. Can you translate this article to get the message out?

Notify of
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments