Timu ya Kuratibu ya Wikimania 2025 inayo furaha kutangaza kwamba Wikimania itafanyika katika kitongoji kidogo cha Gigiri, Nairobi kinachoweza kufikika kwa urahisi. Mkutano huo utafanyika katika kumbi nyingi zilizopo katika eneo la Gigiri ili kuruhusu washiriki kuwa na fursa ya kuzama katika utamaduni wa wenyeji na kupata matoleo mbalimbali.

Gigiri, inayojulikana kwa ukijani kibichi na umaridadi wa kimataifa, ni sehemu yenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa–ofisi pekee ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa barani Afrika na Kusini mwa Dunia–na mashirika mengine kadhaa ya kimataifa na balozi mbalimbali–kitovu cha kweli cha kimataifa na mazingira mwafaka kwa Wanawimedia kukutana na kufahamiana.

Licha ya tabia yake ya kidunia, Gigiri ni eneo dogo-takriban 1km kutoka upande mmoja hadi mwingine. Eneo hilo limejaa mikahawa, maduka ya kahawa, na nafasi tofauti za ununuzi, burudani na shughuli za kijamii, ndani na nje ya Soko maarufu la Village Market.
Wakati wa Wikimania kuanzia tarehe 06-09 Agosti na siku ya kabla ya mkutano tarehe 05 Agosti, programu itaratibiwa kwa ukaribu sana ili washiriki waweze kutembea kwa haraka na kwa urahisi kati ya aina za programu na matukio ya kijamii. Baada ya kusajiliwa, watakaohudhuria watapokea maelezo kamili ya tukio, ikijumuisha ratiba na maeneo ya sehemu mahususi za programu.
Mwaka huu, idadi ya washiriki wa ana kwa ana itakuwa chini kidogo, kwa hivyo tunapendekeza ujisajili mapema ili kujiwekea nafasi. Usajili utafunguliwa mwezi ujao, kwa hivyo kaa chonjo! Kwa usaidizi wa mipango ya usafiri, jisikie huru kuwasiliana na wikimania@wikimedia.org na utembelee Wikimania Wiki ili kugundua punguzo la bei kwenye hoteli na safari za ndege.
Tuna hamu kubwa kuonana nawe jijini Nairobi!

Can you help us translate this article?
In order for this article to reach as many people as possible we would like your help. Can you translate this article to get the message out?
Start translation