Muongo mmoja wa uboreshaji thabiti wa zana ya Kutafsiri Maudhui wazaa zaidi ya makala milioni mbili za Wikipedia

Translate this post

Fikiria umesimama kwenye chumba chenye giza na mshumaa mmoja. Unapogusa mwale wa mshumaa mmoja hadi mshumaa mwingine ambao haujawashwa, giza hupungua zaidi, huku mwale wako wa asili ukiendelea kuwaka sana. Tendo hili linafanana na methali ya kale ya Kiitaliano: “Mshumaa mmoja haupotezi chochote kwa kuwasha mwingine.” Sitiari hii inaonyesha mojawapo ya uvumbuzi wa mageuzi ya Wikipedia—zana ya Kutafsiri Maudhui. Jinsi mishumaa inavyoangaza, zana hii imesaidia “kuwasha” zaidi ya makala milioni 2.4 zilizotafsiriwa katika lugha mbalimbali ndani ya Wikipedia.

Picha ya skrini ikionyesha idadi ya makala yaliyotafsiriwa kwa kutumia zana ya Kutafsiri maudhui.

Kabla ya kuzinduliwa kwa zana ya Kutafsiri Maudhui, pengo kubwa la maarifa lilikuwepo katika Wikipedia za lugha ambazo hazina uwakilishi. Ingawa matoleo katika Kiingereza na lugha nyingine kuu yalisitawi kwa mamilioni ya makala zilizo na vyanzo vya kutosha, Wikipedia za lugha ambazo hazikuwakilishwa sana zilikumbana na ukweli wa kutisha na idadi ndogo sana ya maudhui yaliyo na vyanzo vya kutosha. Pia maarifa kutoka kwa utafiti wa Scott Hales kuhusu athari na mifumo ya uhariri ya wahariri wa lugha nyingi kwenye Wikipedia ilifichua kwamba wachangiaji wa lugha nyingi ambao ni wazungumzaji asilia wa lugha zisizo na uwakilishi wa kutosha mara nyingi huhariri aina sawa za maudhui kwenye Wikipedia zote mbili. Kwa mfano, lugha za Afrika Magharibi, kama vile Hausa na Igbo, zilikuwa na maudhui machache katika Wikipedia zao, na wachangiaji wa lugha nyingi walifanya kazi ya kupanua ujuzi katika lugha hizo kwa kutafsiri maudhui kutoka kwa Kiingereza na Wikipedia za lugha nyingine kubwa zaidi.

Kwa hiyo, kuwa na lugha moja katika lugha hizi za asili kulizuia kwa kiasi kikubwa ufikiaji wa hekima ya pamoja ya wanadamu. Kwa ufikiaji rahisi na bora kwa zana za kutafsiri, wahariri zaidi wa lugha nyingi wanaweza kuchangia kuboresha msingi wa maarifa na vile vile msingi wa wachangiaji katika lugha yao ya asili.

Picha ya chati ya pao inayoonyesha idadi ya makala yaliyoundwa kwa kutumia na bila zana ya Kutafsiri Maudhui katika eneo la Afrika Magharibi kwa miaka mingi.

Wachangiaji wa lugha mbili walikabiliwa na changamoto katika kutafsiri makala za Wikipedia kabla ya zana ya kutafsiri maudhui. Iliwabidi kunakili maudhui kwenye hati tofauti, kuyatafsiri huku wakizingatia muktadha, na kisha kuyaweka katika muundo na kuyadondoa kwa kutumia Wikitext—wakati wote wakifuata sera za uhariri. Mchakato huu mzito ulizuia ushiriki wa watu wa kujitolea, hasa katika Wikipedia za lugha ambazo hazijawakilishwa sana ambapo ujuzi wa kidijitali mara nyingi huwa mdogo. Kuandika makala kutoka mwanzo katika lugha hizo pia kulichukua muda.

Utangulizi wa zana ya Kutafsiri Maudhui

Zana ya Kutafsiri Maudhui, iliyozinduliwa na Shirika la Wikimedia Foundation mnamo 2015, iliendesha mchakato wa kuchosha kiotomatiki, na kuufanya uwe rahisi kwa wingi wa maarifa ya Wikipedia kutiririka katika lugha kwa mchakato wa ukaguzi wa kibinadamu, kuhakikisha uhifadhi wa muktadha ambao unafafanua Wikipedia kama inavyoangaziwa na wazungumzaji wa Kikatalani katika majadiliano ya mezani. Kwa miaka mingi, kwa vile timu ya Wikimedia ya Lugha na Ujanibishaji wa Bidhaa (iliyokuwa timu ya Lugha) imeboresha na kuzidisha zana mara kwa mara, tumeshuhudia ukuaji wa ajabu katika uundaji wa maudhui katika lugha zenye uwakilishi mdogo, na hivyo kuchangia usawa wa maarifa. Muhimu zaidi, pengo la maarifa katika Wikipedia sio tu kuhusu idadi ya vifungu lakini pia utofauti wa mada zinazoshughulikiwa. Hapo awali, matoleo ya Wikipedia Kusini mwa Asia na Afrika Magharibi yalikuwa na sifa ya kuzingatia maingizo ya kijiografia na wasifu, na kuacha masomo muhimu katika STEM, utamaduni, na historia ikiwa na uwakilishi mdogo. Chombo hiki kinasaidia hatua kwa hatua kuziba mapengo haya ya mada katika kanda ndogo.

Kuenea kwa maarifa katika mabara yote

Kupitia uwezo wa ushirikiano na jumuiya za watu wa kujitolea za Wikipedia na kampeni zinazotetea usawa wa maarifa, wachangiaji wamepiga hatua kubwa kwa kutumia zana hii kuongeza maudhui na kuongeza idadi na wigo wa makala katika Wikipedia mbalimbali. Mifano itakuwa:

  • Kwa michango mahususi iliyotolewa katika Kiigbo, na Wikipedia za lugha ya Kihausa, zana hii imeunda asilimia 80 ya maudhui yote, ikiangazia mada muhimu kuhusu STEM, utamaduni, historia na jamii, ambazo hapo awali hazikuweza kupatikana kwa lugha hizi. Mhariri wa kujitolea Aliyu kutoka Nigeria alieleza katika makala kwamba kabla ya zana, hakuweza kuhusisha ni vipi ingekuwa kutafsiri makala za afya mwenyewe kutoka kwa Kiingereza hadi Wikipedia ya Hausa.
Chati ya pao ya idadi ya tafsiri zilizochapishwa katika Wikipedia mbalimbali zinazoangazia machapisho katika Wikipedia ya Kiigbo na Kihausa.
Chati za pao zinaonyesha kiwango cha kutegemea zana ya kutafsiri maudhui kwa kuunda makala katika maeneo manne ya mada ndani ya Wikipedia za Kiigbo na Kihausa.

Wikipedia za lugha ya Kihindi (kama vile Kitelugu, Kitamil, Kinepali, Kibengali, Kikannada, Kimarathi, Kiurdu. Wikipedia za lugha ya Kiassam na Kikashmiri) zimeona ukuaji thabiti wa kila mwaka wa makala zilizotafsiriwa. Wikipedia hizi za lugha, ambazo zinazungumzwa sana Kusini mwa Asia, zimepanuka kutoka kwa kutafsiri chini ya makala 11,000 za mada za STEM hadi zaidi ya 59,641 katika muda wa miaka mitatu pekee.

Chati za pao zinaonyesha kiwango cha kutegemea zana ya kutafsiri maudhui kwa kuunda makala katika maeneo manne ya mada ndani ya Wikipedia za Kiigbo na Kihausa.

Wakati wa janga la Covid-19, zana ilisaidia kikosi kazi cha kutafsiri kutengeneza makala za COVID-19 katika mradi wa WikiProject COVID-19 kupatikana katika zaidi ya lugha 130 kwa muda mfupi. Hii ilisaidia kupunguza hatari ya taarifa potofu kuhusu COVID-19 na kutoa taarifa za kuaminika kwa ulimwengu wakati na baada ya kifungo.

Hasa, makala zilizozalishwa kupitia zana ya kutafsiri zimepimwa kuwa na uwezekano mdogo wa kufutwa kuliko zile zilitungwa kutoka mwanzo. Kuonyesha kwamba zinapohaririwa kwa uangalifu na kukaguliwa na wanadamu, matokeo haya yanayosaidiwa na mashine hutoa maudhui ya ubora wa juu katika Wikipedia nyingi za lugha.

Muongo wa maboresho thabiti

Kama vile mtunza bustani anayekuza miche, timu ya Wikimedia ya Lugha na Ujanibishaji wa Bidhaa imekuza zana ya Kutafsiri Maudhui katika muongo mmoja uliopita. Kama methali ya Kichina inavyosema, “Safari ya maili elfu moja huanza na hatua moja.” Uzinduzi wa Bidhaa ya Kima cha Chini uliashiria hatua hiyo ya kwanza—kupanda mbegu katika bustani kubwa ya Wikipedia. Kila uboreshaji umebadilisha zana, na kusababisha maboresho muhimu:

  • Muunganisho wa Tafsiri ya Mashine ya Google (2016) ambao uliharakisha mchakato wa kutafsiri katika Wikipedia za lugha zaidi kwa kujumuisha rasimu za kwanza za kiotomatiki kutoka kwa Google Tafsiri. Unaweza kusoma zaidi kuhusu athari kutoka kwa matokeo ya mtafiti.
  • Uendelezwaji wa Kiolezo na Usimamizi wa Marejeo (2018) ambao ulibadilisha kwa urahisi violezo changamano katika makala ya kisayansi wakati wa tafsiri, kuhifadhi marejeo na uadilifu wa maudhui.
  • Uzoefu wa tafsiri shirikishi ya simu ya mkononi (2021) ambao uliwaruhusu wahariri wengi kufanyia kazi sehemu tofauti za makala sawa kwa wakati mmoja, na kuboresha ushirikiano.

Kufikia 2021, zana hii ilikuwa imebadilika ili kukabiliana na changamoto za kijamii na teknolojia, na kuwa zana thabiti kwa watumiaji wa kompyuta ya mezani na simu ya mkononi kutafsiri kwa ushirikiano makala sehemu baada ya sehemu huku ikigundua matumizi mabaya ya tafsiri ya mashine.

Maendeleo zaidi ya kiufundi yaliendelea kupanua ufikiaji wa zana:

  • Tafsiri ya Mashine ya MinT: Kukuza usaidizi wa tafsiri kwa zaidi ya jozi za lugha 40,000. Iliongeza kiwango cha uzalishaji cha wafasiri katika matoleo 55 ya lugha ya Wikipedia, ambayo yalipata usaidizi wa tafsiri ya MinT kwa mara ya kwanza. Maelezo zaidi yanapatikana katika makala hii.
  • Kipengele cha Pendekezo la Tafsiri Iliyobinafsishwa: Hii ni uboreshaji wa hivi karibuni kutoka kwa timu. Kazi hii imeboresha usaidizi wa orodha ya mapendekezo ya makala ya zana ya kutafsiri Maudhui, ikiwawezesha watumiaji kubadili na kupokea mapendekezo ya makala kulingana na vichujio 41 vinavyotegemea mada. Hii ina maana kwamba wanaweza kugundua na kutafsiri makala katika maeneo yanayowavutia na utaalamu wao, na pia kugundua orodha zilizoratibiwa na jumuiya zinazoitwa Makusanyiko ambazo zimechochewa na mipango ya kampeni ya kukuza maudhui. Hivi sasa, kipengele hiki kina takriban makusanyo 50 na kuendelea, na uboreshaji zaidi yapo njiani.
  • Dashibodi iliyounganishwa ilifanya iwe rahisi kufikia uwezo sawa kwenye kompyuta ya mezani na vifaa vya mkononi. Kwa hili, watumiaji wa kompyuta ya mezani walipewa uwezo wa kutafsiri makala sehemu kwa sehemu, na vichujio vilivyo binafsishwa ili kupata mapendekezo ya tafsiri ambayo yanalingana na eneo lao pendwa.
Ramani ya uboreshaji wa zana hii inaonyesha maendeleo na inasisitiza falsafa: kurudia mara kwa mara, kwa kufikiria na maboresho ya ziada husababisha matokeo makubwa kwa wakati, kujaza bahari ya uwezekano hatua kwa hatua.

Jukumu lako katika usawa wa maarifa

Mabadiliko ya zana hii yanaonyesha wajibu wa maendeleo endelevu, kupanua ufikiaji wa habari za hali ya juu, zilizopitiwa na mwanadamu katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na STEM, Utamaduni, na Historia. Kila makala iliyotafsiriwa huunda miunganisho mipya na kuhimiza watu zaidi kushiriki katika juhudi hizi za kimataifa. Hivi ndivyo unavyoweza kuhusika:

Kwa Wahariri wa Lugha Nyingi: Tumia zana ya Kutafsiri Maudhui kutafsiri makala katika lugha unazozijua. Hata makala moja inaweza kumsaidia mtu kupata taarifa katika lugha yake ya asili.

Kwa waandaaji wa kampeni za ukuaji wa maudhui: Andaa matukio ya kutafsiri yanayolenga mada muhimu kwa lugha zilizo na uwakilishi mdogo na tumia kishikizo cha ukusanyaji wa ukurasa kuvutia watafsiri zaidi kutafsiri orodha ya makala zako.

Zana ya Kutafsiri Maudhui inaonyesha wajibu wa Wikipedia kufanya maarifa yapatikane kwa kila mtu. Kwa pamoja, tunaweza kusaidia kwa kutoa maarifa na njia za mwanga kwa wengine ili kupanua udadisi na uelewa kwa wote.

Can you help us translate this article?

In order for this article to reach as many people as possible we would like your help. Can you translate this article to get the message out?