Usajili kwaajili ya Mkutano wa Wikimania 2025, utakaofanyikia jijini Nairobi, Kenya, na mtandaoni, sasa umefunguliwa! Jiunge nasi kuanzia Agosti 6 hadi Agosti 9 tukiwa tunaadhimisha miaka 20 ya Wikimania.
Mwaka huu, uwezo wa kuhudhuria ana kwa ana umepunguzwa kidogo, kwa hivyo tunapendekeza ujisajili mapema ili kuhakikisha unapata nafasi. Usajili wa tukio la ana kwa ana utakuwa wazi mpaka tarehe 13 Julai au pale nafasi zitakapokuwa bado zipo. Kwa uzoefu wa ushiriki wa mtandaoni kwenye Eventyay, jukwaa letu la matukio mtandaoni la programu huria, utaweza kujisajili wakati wowote.
Shughuli jijini Nairobi zitaanza tarehe 5 Agosti kwa siku ya kabla ya Mkutano itakayojumuisha mikusanyiko mingi na matukio ya kijamii, ikijumuisha mkutano maalum kwa watumiaji walio na haki za ziada, Mkutano wa WikiWomen, na ziara za kitamaduni za jiji na mazingira yake kwa wale wanaotaka kuzuru Nairobi.
Kuanzia Agosti 6–9, mkutano mkuu utafanyika katika maeneo kadhaa ndani ya Gigiri, Nairobi, kitongoji kidogo na salama kinachojulikana kwa tabia yake ya kimataifa na kupakana na msitu mzuri wa Karura. Vikao, warsha, na mikutano yote itakuwa ndani ya matembezi mafupi kutoka kwa kila kimojawapo.
Baada ya kujisajili, utapokea maelezo yote—ratiba kamili, ramani za maeneo na kila kitu unachohitaji ili kufaidika zaidi na uzoefu wako wa Wikimania.Nairobi ina maeneo mengi unayoweza kuchagua kwaajili ya malazi. Tumeingia ubia na hoteli za karibu ili kuwapa washiriki wa Wikimania punguzo la bei la kipekee. Angalia ofa bora za hoteli karibu na Wikimania ukitumia ramani hii shirikishi. Kuna mashirika machache ya ndege washirika ambayo yanatoa punguzo la nauli ya ndege kwa washiriki wa Wikimania wanaosafiri kwenda na kutoka Nairobi (NBO).
Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kujiandaa kwa safari yako, jinsi ya kuzunguka Nairobi, na jinsi ya kutumia vyema wakati wako nchini Kenya, soma mwongozo wa safari ambao tumekuandalia! Ikiwa una maswali yoyote, jisikie huru kututumia barua pepe kwenda wikimania@wikimedia.org.
Kumbuka: tiketi ya kuhudhuria mkutano huu ana kwa ana inafadhiliwa na Shirika la Wikimedia Foundation na inagharimu $100 USD, ambayo inagharamia matukio ya ufunguzi na kufunga, pamoja na chakula cha mchana katika siku kuu za mikutano. Wapokeaji wa Ufadhili watapokea nambari za kuthibitisha ili kujiandikisha kwa tukio la ana kwa ana. Kongamano la mtandaoni linafadhiliwa kikamilifu na Shirika na litaendelea kubaki bila malipo kwa watakaohudhuria.
Taarifa ya faragha ya usajili.
Karibu Nairobi
Nairobi ina maeneo mengi unayoweza kuchagua kwaajili ya malazi. Tumeingia ubia na hoteli za karibu ili kuwapa washiriki wa Wikimania punguzo la bei la kipekee. Angalia ofa bora za hoteli karibu na Wikimania ukitumia ramani hii shirikishi. Kuna mashirika machache ya ndege washirika ambayo yanatoa punguzo la nauli ya ndege kwa washiriki wa Wikimania wanaosafiri kwenda na kutoka Nairobi (NBO).
Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kujiandaa kwa safari yako, jinsi ya kuzunguka Nairobi, na jinsi ya kutumia vyema wakati wako nchini Kenya, soma mwongozo wa safari ambao tumekuandalia! Ikiwa una maswali yoyote, jisikie huru kututumia barua pepe kwenda wikimania@wikimedia.org.
Kumbuka: tiketi ya kuhudhuria mkutano huu ana kwa ana inafadhiliwa na Shirika la Wikimedia Foundation na inagharimu $100 USD, ambayo inagharamia matukio ya ufunguzi na kufunga, pamoja na chakula cha mchana katika siku kuu za mikutano. Wapokeaji wa Ufadhili watapokea nambari za kuthibitisha ili kujiandikisha kwa tukio la ana kwa ana. Kongamano la mtandaoni linafadhiliwa kikamilifu na Shirika na litaendelea kubaki bila malipo kwa watakaohudhuria.
Taarifa ya faragha ya usajili.

Can you help us translate this article?
In order for this article to reach as many people as possible we would like your help. Can you translate this article to get the message out?
Start translation