Uzoefu wangu katika Mkutano wa Watumiaji wenye hazi za ziada – Wikimania 2025, Nairobi, Kenya

Translate this post

Kuhudhuria mjadala wa ana kwa ana wa Watumiaji wenye haki za ziada katika mkutano wa Wikimania 2025 hapo Nairobi umeleta hisia za furaha na kushangaza kwa pamoja. Kama mtu ninayetokea kwenye jamii ndogo, imekua ni hamasa mno kukutana na watu mbalimbali wanaofanya kazi bila kuchoka kuhakikisha elimu inakua huria na kupatikana kwa usawa. Kukutana na nyuso zilizo nyuma ya michango katika miradi hiyo, kukutana na watu kutoka katika Mazingira tofautitofauti ilikua ni jambo ambalo sitolisahau katika safari yangu ndani ya Wikimedia.

Muda wote wa mkutano, nimepata fursa ya kujifunza kuhusu miradi ya Wikimedia kidunia, vitendea kazi na mipango mbalimbali kusaidia lugha ndogo kama yangu. Sana sana nilivutiwa na vipindi kuhusu Wiki – ndogondogo na namna gani Watumiaji wenye haki za ziada wanapambana kuhakikisha wanaboresha maudhui na upatikanaji wake.

Masomo Muhimu

Baadhi ya masomo muhimu niliyojifunza ni pamoja na umuhimu wa ushirikiano wa kanda mbalimbali, umuhimu wa masimulizi ya hadithi katika utengenezaji wa maudhui, na uhitaji wa mwendelezo katika kuihusisha na kuishirikisha jamii. Pia nimejifunza umuhimu wa kuunganisha mifumo ya maarifa ya wenyeji – kama vile masimulizi ya njia ya mdomo katika mchango wetu wa kidijitali, hasa katika lugha ambazo hazijawakilishwa vizuri. Kilicho muhimu zaidi, niligundua kuwa kila mchango unaofanywa na mtumiaji mwenye haki za ziada, bila kujali anapotoka au ukubwa wa jamii yake, ni wa maana katika dhamira pana ya kuhakikisha maarifa huru kwa wote.

Matarajio

Kuendelea mbele, nimejitoa zaidi kuliko mwanzo kuendeleza hii kazi – kuimarisha ushiriki wa jamii za wenyeji, kukuza utofauti wa lugha na kujenga mahusiano thabiti kabisa na harakati za Wikimedia duniani. Wikimania 2025 imenikumbusha kuwa hata jamii ndogo zina sauti muhimu katika mfumo wa maarifa huria.

Can you help us translate this article?

In order for this article to reach as many people as possible we would like your help. Can you translate this article to get the message out?