Dirisha la maombi ya ufadhili wa kuhudhuria mkutano wa Wikimania 2026 huko Paris sasa liko wazi!

Translate this post

Fungasha bereti zako na kuwa tayari kushika njia kuyaelekea maarifa, Wikimania 2026 inakuja hapo Paris

Kuanzia 21–25 Julai 2026, Jiji la Mataa/Jiji la Nuru litawakutanisha Wanawikimedia kutoka pande zote za dunia kwa siku tano za mawasiliano, ushirikiano na sherehe. Ni wapi pengine pazuri pa kuchanganya historia, utamaduni na mawazo yanayobadilisha dunia kuliko Paris, ambako mapinduzi, uvumbuzi na hamasa vimekuwa hewani kwa karne nyingi?

Tangazo la picha mjongeo kuhusu Wikimania 2026 Paris.

Mwaka huu ni wa kipekee zaidi kwa sababu Wikipedia inatimiza miaka 25! Kwa muda wa robo karne, washiriki wanaojitolea kila mahali wamekuwa wakijenga chanzo kikubwa zaidi cha maarifa ya bure katika historia. Wikimania Paris itakuwa jukwaa kamili la kusherehekea mafanikio haya ya ajabu na kuota ndoto kubwa zaidi kwa miaka 25 ijayo.

Mada yetu: Uhuru, Usawa na Uaminifu

Mada ya mwaka huu ni: ”Uhuru, Usawa, Uaminifu” , siyo tu kauli mbiu. Ni wito wa kuchukua hatua. Katika dunia ambapo maarifa yanakabiliwa na hatari zinazotokana na siasa, vyombo vya habari, na teknolojia, miradi ya Wikimedia inabaki kuwa ni nafasi chache salama za kushirikiana maarifa kwa uhuru, kwa ushirikiano, na kwa uaminifu.

  • Uhuru unamaanisha haki ya kushiriki, kujieleza, kuhariri, na kubuni kwa usalama. Ni uhuru wa kushirikisha maarifa bila hofu, na kuhakikisha kila sauti inasikika.
  • Usawa unahakikisha kila mtu, bila kujali asili au rasilimali, ana njia za kuchangia na kupata maarifa. Ni juu ya kujenga encyclopedia ya dunia yenye utofauti, ushirikishi, na inayowakilisha kila mtu.
  • Uaminifu ni ahadi yetu kwa maudhui yenye ukweli, usawa, na yanayoweza kuthibitishwa. Katika zama za taarifa zisizo sahihi, miradi ya Wikimedia ni taa ya taarifa za kuaminika kwa kila mtu, kuanzia wanafunzi, waandishi wa habari, hadi waendelezaji wa akili mnemba (AI).

katika Wikimania ya Paris, tutachunguza maadili haya pamoja, kuimarisha jamii zetu, na kuchukua hatua za kulinda upatikanaji wa bure wa maarifa duniani kote.

Timu ya Waandaaji wa Wikimania 2026 katika sherehe ya kufungwa kwa Wikimania 2025 huko Nairobi.

Tuma maombi ya Ufadhili sasa!

Maombi ya Ufadhili yanafunguliwa tarehe 10 Septemba, 2025! Ikiwa ungependa kuhudhuria Wikimania huko Paris, ufadhili huo upo kufadhili usafiri, malazi, na usajili. Yako wazi kwa Wanawikimedia wote, na tunawahimiza wale kutoka jamii zisizowakilishwa vya kutosha kuomba.

Tuma maombi hapa kabla ya tarehe 31 Oktoba, 2025, na wale watakaokubalika watajulishwa mnamo Januari 2026. Kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma, washiriki watakaohudhuria wataombwa kujitolea kwa masaa 4–6 wakati wa Wikimania, na wakiwa na chaguo la kujitolea zaidi ikiwa wanataka. Washindi wote wa ufadhili huu pia wanadhaminiwa chini ya Sera ya Bima ya Usafiri ya Wikimedia Foundation.

Ili kukusaidia na maombi yako ya ufadhili, kutakuwa na muda wa ofisi uliopangwa kukuelekeza kupitia mchakato huu. Endelea kufuatilia taarifa na soma zaidi kuhusu mada hapa. Ikiwa una maswali yoyote, usisite kuwasiliana na timu ya waandaaji kupitia wikimania-scholarships@wikimedia.org.

Usikose fursa hii ya kusherehekea miaka 25 ya Wikipedia katika Jiji la Nuru, kuungana na Wanawikimedia kutoka duniani kote, na kuwa sehemu ya kuunda mustakabali wa maarifa ya bure. Paris inakusubiri—na washiriki wenzako pia!

Angalia Taarifa ya Faragha ya Maombi ya Ufadhili.

Can you help us translate this article?

In order for this article to reach as many people as possible we would like your help. Can you translate this article to get the message out?