Kujifunza kuhusu Wikimedia barani Afrika

Translate this post

Je, unajua ni wapi harakati za Wikimedia zinakua kwa kasi zaidi duniani?

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kumekuwa na ukuaji mkubwa wa harakati za Wikimedia barani Afrika, kama inavyoonekana kutokana na kuongezeka kwa idadi ya Vikundi vya Watumiaji, wageni na ushiriki wa kanda katika matukio ya harakati na miradi.

Kukuza usawa wa maarifa kupitia mafunzo ya kina ya kikanda

Upanuzi huu na ongezeko la shughuli barani Afrika unawiana na nguzo mbili za Mwelekeo wa Kimkakati wa harakati, usawa wa maarifa na maarifa kama huduma. Mwaka huu, kama sehemu ya Mpango wa Mwaka wa Wikimedia Foundation, tulianzisha msisitizo wa kazi za kikanda kama sehemu ya dhamira yetu wenyewe ya kuendeleza usawa wa maarifa na kusaidia mkakati wa harakati. Sisi sote ni sehemu ya harakati za kimataifa zinalohusisha maeneo, lugha na jamii, na lengo hili la kikanda litaruhusu Shirika kuelewa vyema mahitaji ya ndani na mienendo ya kikanda kama sehemu ya kazi yetu.

Tulizindua mbinu hii mpya mwanzoni mwa mwaka huu wa fedha kwa kuboresha uratibu wetu katika ngazi ya kanda. Timu za shirika zinazofanya kazi katika maeneo na kushirikiana na jamii za wenyeji sasa hukutana kimakusudi zaidi kubainisha matokeo ambayo kwa pamoja tunaweza kuleta katika maeneo mbalimbali ya dunia. Kila robo, tutakutana ili kujadili mienendo na shughuli za kikanda na kihistoria za watu binafsi wa kujitolea, Matawi, Vikundi vya Watumiaji, Mashirika ya Mada, mashirika ya wash irika katika mfumo wa maarifa bila malipo. Vikao hivi ni ukaguzi muhimu kama sehemu ya Mpango wetu wa Mwaka, na huangalia kazi iliyopangwa na timu mbalimbali katika Shirika ili kuweka kipaumbele na kuoanisha rasilimali kwa matokeo lengwa na ushirikiano wenye matokeo zaidi. Hapa kuna mafunzo yetu kwa Afrika.

Wikimedia barani Afrika

Ukuaji mkubwa katika vikundi vya watumiaji wa Kiafrika na washirika

Ingawa Afrika Kusini bado ni tawi pekee barani Afrika tangu kuunganishwa kwake mnamo 2012, eneo hilo lina idadi kubwa ya Vikundi vya Watumiaji, ambavyo baadhi yao vimeundwa vyema na vinaendeshwa sawa na matawi katika maeneo mengine. Washirika katika eneo la Afrika wameongezeka kutoka Washirika 6 mnamo 2014 tulipoandaa Wiki Indaba yetu ya kwanza huko Johannesburg Afrika Kusini hadi washirika 21.

Urahisi wa kuunda Kikundi cha Watumiaji ikilinganishwa na Matawi ndio huhamasisha jamii nyingi barani Afrika kuchagua ya kwanza kama mahali pa kuanzia. Baadhi ya Vikundi vipya vya Watumiaji katika eneo hili, ambavyo vimetambuliwa rasmi hivi karibuni na Kamati ya Ushirikiano ni pamoja na; Dagbani Wikimedians User GroupGungbe Wikimedians User GroupWikimedia Community User Group RwandaWikimedia User Group KenyaWikimedians of Lagos User Group na Tyap Wikimedians User Group. Jamii nyingi katika eneo hilo zimejikita katika miradi inayohusu utamaduni na lugha za wenyeji.

Video kuhusu matokeo  ya Harakati za Wikimedia barani Africa – sehemu ya mfululizo wa Behind the Screen
 

Msaada kwa harakati

Ikiwa na zaidi ya watu bilioni moja na zaidi ya nchi 450+, Afrika inawakilisha mojawapo ya kanda changa zaidi duniani – 97% ya watu ni chini ya miaka 65 na ongezeko hili la ghafla la vijana linaonekana katika harakati. Hata hivyo kuna nafasi ya ukuaji katika eneo hili kwani Afrika inawakilisha 1% pekee ya wahariri hai wa kipekee duniani kote licha ya kuwa na 7% ya watumiaji wa mtandao duniani.

Kwa bahati nzuri, tayari tunaona mafanikio kadhaa katika eneo hili. Wageni wana uwezekano mara tatu zaidi wa kutoka Afrika, kulingana na data kutoka Ripoti ya Maarifa ya Jamii ya 2020 . Ushirikiano wa kikanda barani Afrika umelenga katika kuendeleza miundo ya ushirikiano ili kuendesha michango ya wageni kwa kuzingatia elimu na kampeni za kujenga uwezo.

Mpango wa Maarifa wa Afrika (AKI), kwa ushirikiano na Umoja wa Afrika (AU) ni mojawapo ya ushirikiano huo ambao unalenga kuongeza kujenga uwezo kwa jamii katika kanda.

Programu ya Rika Kujifunza ya  Let’s Connect, ambayo inaunda nafasi kwa Wanawikimedia kushiriki ujuzi wao na kujifunza kutoka kwa wengine, pia imethibitishwa kuwa njia nzuri ya kujifunza kwa usawa katika harakati. Afrika na Asia zilijumuisha watu wengi waliojiandikisha kwa programu ya Let’s connect, ishara kubwa ya kujitolea kwa eneo hilo sio tu kujifunza bali kushiriki maarifa na wenzao pia.

Pia kumeonekana kuongezeka kwa ushiriki katika kanda ya Afrika katika kampeni za kimataifa kama vile Wiki For Human Rights, ambayo imeona ukuaji wa ajabu barani Afrika. Takribani nusu ya matukio na ushiriki katika kampeni ya #WikiForHumanRights imekuwa na jamii barani Afrika, ambazo pia zinaitumia kushirikiana kwa karibu na mashirika ya mazingira na haki za binadamu.

Jumla ya Ruzuku kwa Mwaka wa Kalenda barani Afrika

Katika miaka kadhaa iliyopita, jamii barani Afrika zimepokea ufadhili zaidi kutoka kwa Shirika. Haya ni matokeo ya mkakati wa Wikimedia Foundation kugatua rasilimali hasa miongoni mwa jamii zenye uwakilishi mdogo.

Katika mwaka wa fedha wa 2021-2022, duniani kote kulikuwa na ongezeko la 51% la ufadhili ikilinganishwa na mwaka uliopita, kutoka milioni 8.2 katika ufadhili hadi milioni 12.4. Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika (MEA) ilipata ongezeko la 279% mwaka huu – kutoka USD $784,951 hadi $2,189,257 katika mwaka wa fedha wa 2021-22.

Mfuko wa  Fedha za Msaada wa Jumla ziliunda sehemu kubwa zaidi ya ufadhili kwa 59% ikifuatiwa na Mfuko wa Fedha za Haraka 30% na hazina ya Mwungano wa Wikimedia kwa 10%. 100% ya jumla ya uwekezaji katika eneo hili ilikuwa kwa jamii zinazoibuka.

Nchi za Kiafrika pia zilionyesha uwiano wa juu zaidi ya wastani wa “mwonekano wa ukurasa kwa kifaa kinachotumika” katika programu ya Android, ikilinganishwa na ulimwengu wote. Hii ina maana kwamba mtumiaji fulani wa programu ya Android barani Afrika anasoma kurasa nyingi zaidi kuliko watumiaji wa programu duniani kote. Ya juu Zaidi ni Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ghana, na Nigeria.

Usaidizi wa utafsiri wa mashine pia ulitolewa kwa mara ya kwanza katika Tafsiri ya Maudhui/Sehemu kwa lugha ya Kiganda. Wahariri wa Kiluganda walitoa maoni chanya kuhusu ubora wa tafsiri zinazotolewa na zana hii. Ubunifu huu unaweza kusaidia kukuza maarifa bila malipo katika Wikipedia za lugha mpya na ndogo kote barani Afrika. Shirika lilishirikiana na jamii tisa zisizo na usaidizi wa kutafsiri kwa machine kwa lugha zao (Kiwolof, Iloko, Kikongo, Kilingala, Kisotho cha Kaskazini, Kiswati, Kitswana, Kioromo na Kitigrinya).

Kuanzia tarehe 4-6 Novemba, Wanawikimedia na washirika kote barani Afrika watakutana pamoja kusherehekea mafanikio haya na kushiriki mafunzo katika WikiIndaba, mkutano wa kikanda wa Waafrika ndani ya Afrika na nje ya nchi. Mkutano huu utalenga kujenga uwezo kwa Wanawikimedia wa Kiafrika, kukuza ukuaji wa utangazaji na ushiriki wa Afrika katika miradi ya Wikimedia, kuunganisha Wanawikimedia wa Kiafrika ndani ya bara na katika diaspora, na kubadilisha mawazo kuwa vitendo kulingana na mada ya mkutano wa 2022; “Kuendeleza Ajenda ya Afrika katika Mkakati wa Harakati wa 2030”.

Tusaidie kujifunza

Je, hii inakosa kitu? Acha maoni hapa chini na utuambie kuhusu kazi kubwa katika kanda.

Can you help us translate this article?

In order for this article to reach as many people as possible we would like your help. Can you translate this article to get the message out?