Kaa chonjo kwa mijadala ya jumuiya kuhusu Baraza la Kimataifa na Hebu

MCDC members in Utrecht meeting June. 2023. CC BY-SA 4.0, Wikimedia Commons
Wajumbe wa MCDC Katika kikao huko Utrecht mnamo June 2023, CC BY-SA 4.0 kupitia Wikimedia Commons. Mwanachama wa MCDC Pepe Flores hakuwepo wakati huo.

Kuanzia tarehe 2 hadi 4 Juni 2023, Kamati ya Uandishi wa Mkataba wa Harakati (MCDC) ilikusanyika Utrecht, Uholanzi, kufanyia kazi sura muhimu za Mkataba wa Harakati za Wikimedia: Baraza la Kimataifa, Ufanyaji Maamuzi, Hebu, Kazi & Majukumu, na Faharasa.

Kila mwanachama wa MCDC amekuwa akitoa muda wake wa thamani tangu 2021 kutimiza wajibu wao wa pamoja wa kuandaa hati ya vuguvugu la Wikimedia. Sasa, ni wakati wa vuguvugu la kuunga mkono MCDC katika kutoa hati ambayo ina tija, kwa kuzingatia maono yetu ya pamoja na kanuni, na kuweka mkakati wa 2030. Wajibu unashirikishwa na wakati uliokuwa unasubiriwa kwa hamu wa jamii kushiriki kikamilifu kuhusu rasimu ya Mkataba wa Katiba ya Harakati umefika. Angalia hatua zinazofuata hapa chini na ujue jinsi wewe na wanajumuiya wako mnavyoweza kushiriki! 

Sherehe, nyakati tata na umoja wa wanatimu: mada kubwa za kuzingatia

Wajumbe wa MCDC wakipiga kura juu ya matokeo ya mjadala, June 2023, CC BY-SA 4.0 kupitia Wikimedia Commons

Ingawa wanashirikiana mara kwa mara mtandaoni, hii ilikuwa mara ya tatu tu kwa wajumbe wa MCDC kupata fursa ya kukutana pamoja na kufanya kazi ana kwa ana. Vikao hivyo vilizingatia matokeo, vikikuza fikra za pamoja, na kuhimiza maelewano ya watu binafsi kufikia upatanishi. Kwa kuzingatia majadiliano ya kimataifa yajayo ya jumuiya ya kimataifa yatakayojikita katika sehemu kubwa zaidi ya Mkataba: Baraza la Kimataifa, Ufanyaji Maamuzi, Hebu, Kazi na Wajibu, na Faharasa, MCDC ilikubali kukumbatia “Kizuri vya kutosha” badala ya kujitahidi kupata ukamilifu ili kuendelea. kwenye uandishi wao. Ni kwa mrejesho na maoni ya jumuiya pekee ambapo rasimu za Mkataba wa Harakati zinaweza kubadilika zaidi na baadae kuidhinishwa na harakati.

MCDC ilibidi ikubaliane kwa pamoja kuhusu baadhi ya mada muhimu kuhusu Baraza la Kimataifa na Hebu. Walijadili madhumuni ya Baraza la Kimataifa na majukumu yake linapokuja suala la rasilimali za harakati, muundo, na uanachama, miongoni mwa mengine. Kwa Hebu, majadiliano yaligusa ufafanuzi na madhumuni, uanachama na muundo, usanidi na michakato ya utawala. Mazungumzo ya ana kwa ana yaliyowezeshwa yaliharakisha sana mchakato wa kufikia makubaliano kuhusu mambo muhimu yanayohusu Baraza la Kimataifa na Hebu.

Juhudi za kihistoria

Mjumbe wa MCDC Runa Bhattacharjee akiwasilisha majibu ya mjadala, CC BY-SA 4.0 kupitia Wikimedia Commons

Wazo la kuanzisha shirika la kimataifa ambalo litawakilisha jumuiya mbalimbali na kuleta mabadiliko ya kimuundo limekuwa mada ya mjadala katika vuguvugu la Wikimedia tangu mapema mwaka wa 2005.

Mojawapo ya mapendekezo ya awali ilikuwa WikiCouncil mwaka 2005. Madhumuni yalikuwa kuwa chombo cha uwakilishi kwa miradi yote ya Wikimedia na kufanya kazi pamoja na Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Wikimedia (BoT). Sababu ya pendekezo la kikundi ilikuwa kusaidia miradi ya ndani, kuboresha mawasiliano, na kuwezesha jamii. Hakukuwa na makubaliano juu ya haja ya Baraza kama hilo wakati huo mapema sana katika safari yetu ya wiki. Kulikuwa na wasiwasi juu ya kuongeza urasimu na utata wa kujitahidi kwa uwakilishi. Wasiwasi huu umesalia hadi leo ingawa harakati zetu zimekua kwa njia zilizotarajiwa na ambazo hazijawahi kufanywa kote ulimwenguni na hitaji la usawa katika kufanya maamuzi tangu wakati huo limeelezwa wazi.

Juhudi pangifu zaidi zilifanywa mwaka wa 2010 wakati wa Mradi wa Majukumu ya Harakati. Juhudi hizo zililenga kuchunguza na kufafanua majukumu mbalimbali ndani ya harakati za Wikimedia na jinsi yanavyochangia katika dhamira ya jumla. Kama matokeo ya Mradi wa Majukumu ya Harakati, Modeli ya Ushirikiano ilitengenezwa: ukiachilia mbali mashirika, vikundi vya watumiaji na mashirika ya kimada pia yakawa aina zinazowezekana za vyombo vya Wikimedia. “Kamati ya Mashirika” iliyopita ilipanuliwa katika wigo na kupata Kamati ya sasa ya Ushirikiano.

Mradi wa Majukumu ya Harakati pia ulipendekeza hati ya harakati kwa madhumuni ya kusaidia harakati kukua kama mtandao wenye nguvu wa kimataifa ili kufikia dhamira yake, kwa matumaini kwamba katiba hiyo ingesaidia harakati na kuongeza ufikiaji wake kwa sehemu za ulimwengu zilizo na uwakilishi mdogo. Mkataba ulibakia katika hatua ya rasimu ya sehemu na haukukamilika. Mawazo mengi yaliyotolewa katika mradi huu yaliathiri mapendekezo ya Mkakati wa Harakati wa 2030, ikiwa ni pamoja na utayarishaji wa Mkataba wa Harakati unaoendelea.

Mnamo 2012, wakati wa Mkutano wa Wikimedia huko Berlin, wanachama wa mashirika 30 walikusanyika ili kuanzisha Jumuiya ya Mashirka ya Wikimedia. Chama kiliundwa na mwakilishi mmoja kutoka kila shirika na mtu mmoja kwa pamoja akiwakilisha makundi yote ya watumiaji. Ilikusudiwa kusaidia zaidi ubadilishanaji wa maarifa na ushiriki wa washirika. Mwaka mmoja baada ya mkutano wake wa kwanza, halikufanyika kwa ufanisi kutokana na masuala mengi, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa makubaliano juu ya madhumuni ya Chama, majukumu yake kamili ya utendaji, na nafasi ya ofisi. Miaka miwili baadaye, Mjadala wa Chapta ilikuwa jitihada kubwa ya kusikiliza mahitaji, malengo, na uzoefu wa Chapta za Wikimedia. Baadhi ya masuala muhimu ambayo yalijitokeza mwaka wa 2013 bado ni muhimu au yanabaki kufikirisha hadi leo, ikiwa ni pamoja na haja ya uongozi katika harakati.

Mnamo 2017, mwelekeo wa kimkakati uliundwa ili kuongoza harakati zetu katika siku zijazo: Kufikia 2030, Wikimedia itakuwa miundombinu muhimu ya mfumo ikolojia wa maarifa ya bure, na yeyote anayeshiriki maono yetu ataweza kujiunga nasi. Kuanzia 2018 hadi 2020 watu kutoka pande zote walikusanyika ili kuunda mapendekezo ya Mkakati wa Harakati na kanuni elekezi. Uundaji wa Mkataba wa Harakati na Baraza la Kimataifa unatokana na pendekezo la 4 la Mkakati wa Harakati: “Kuhakikisha Usawa katika Ufanyaji Maamuzi“. Hapo awali, ilipendekezwa kuwa Baraza la Muda la Ulimwenguni (IGC) lingesimamia uanzishwaji wa Mkataba wa Harakati na Baraza la Kimataifa. Katika mchakato huo, jukumu la IGC la kuandaa Mkataba wa Harakati lilihamishiwa kwa Kamati ya Uandishi wa Mkataba wa Harakati. Jitihada za MCDC zimetokana na majaribio ya awali ya kuunda hati, dira ya Mkakati wa Harakati wa 2030, na ujuzi wao wenyewe na ujuzi kutoka kwa jumuiya mbalimbali.

Kifuatacho? 

Wajumbe wa MCDC wakifanya zoezi la kuoanisha la 3D katika makundi madogo madogo, CC BY-SA 4.0 kupitia Wikimedia Commons

Kuna maswali na hoja za majadiliano ambazo zinahitaji maoni kutoka kwa jumuiya pana ili kuhakikisha kwamba mwishoni, Mkataba ni matokeo ya juhudi za ushirikiano wa harakati zetu za kimataifa. Mazungumzo ya jumuiya yatafanyika kuanzia Julai hadi Septemba. Sura mpya zitashirikishwa kwenye Meta katika vijipande pande ili kutenga muda wa kutosha kwa Harakai za Wikimedia kuzoea maandishi. 

 Watu binafsi au vikundi kutoka jumuiya za lugha ambazo hazina nyenzo za kutosha wanaalikwa kutuma maombi ya ruzuku ili kuandaa mijadala katika lugha zao. Wataalamu wa Kikanda wa Timu ya Mawasiliano ya Harakati watakuwa wa msaada kwa waandaaji wa jumuiya yoyote.

Ratiba ya mazungumzo yajayo ya jumuiya itatangazwa mapema Julai. MCDC inapanga kutumia mikusanyiko iliyopo ya jamii ili kusikiliza harakati za Wikimedia. Ikiwa ungependa kuanzisha mjadala kuhusu Mkataba wa Harakati katika jumuiya yako, tafadhali wasiliana na timu ya usaidizi kupitia movementcharter@wikimedia.org au kwenye ukurasa wa mazungumzo wa Meta.

Tunatumai kukuona katika mazungumzo ya jumuiya.