Tamasha la Wikimania linafanyika kimataifa

Kuanzia 11-14 Agosti, Tamasha la Wikimania litazileta pamoja jumuiya kutoka ulimwenguni kote kusherehekea ufikiaji bure na wa wazi wa maarifa. Kwa kutumia njia inayolenga maeneo ya kikanda, tunatumai kuwakaribisha wachangiaji wengi zaidi kwenye tamasha hili la kipekee na la kimataifa la harakati zetu.

Usajili utafunguliwa hivi karibuni!  Hizi hapa taarifa za kuchungulia kuhusiana na namna Tamasha litakavyoweza kuwaunganisha wenyeji na ulimwengu.

Kuzileta Kanda pamoja wakati wa Tamasha la Wikimania

Tamasha la Wikimania litakuwa na programu zinazozunguka kati ya kanda tatu za longitudi: Asia-Oceania; Marekani; na Afrika, Ulaya na Mashariki ya Kati.  Kila siku itapangiliwa ili kuwezesha ushiriki wa watu wa eneo husika, na itapangiliwa ili kuongeza mwingiliano na saa za maeneo mengine. Kila siku itaangazia jumuiya mahalia na za kikanda zinazofanya kazi ndani ya eneo hilo. Tunategemea kila siku kuwa ya kipekee na ya kufurahisha, ili kuwaruhusu washiriki wa Wikimania kuwa na maono mapana kuhusiana na mabadiliko, mienendo, na michango ya maeneo mbalimbali kwa upana wake katika harakati. Kila siku itaangazia lugha za nyongeza za eneo husika na itaangazia jumuiya mahalia na za kikanda zinazofanya kazi ndani ya eneo hilo. Tunategemea kila siku kuwa ya kipekee na ya kufurahisha, ili kuwaruhusu washiriki wa Wikimania kuwa na maono mapana kuhusiana na mabadiliko, mienendo, na michango ya maeneo mbalimbali kwa upana wake katika harakati.

Kutoka lugha saba hadi kumi na tatu: kukaribisha jumuiya nyingi zaidi kuliko hapo awali

Mwaka jana ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kwa mkutano wa Wikimania kutafsiriwa kwa lugha mbalimbali. Mwaka huu, karibia tunazidisha mara mbili idadi ya lugha zitakazopewa usaidizi wa tafsiri kwa tukio hili la mtandaoni: kutoka saba hadi kumi na tatu. Kama nyongeza kwa lugha kuu za Umoja wa Mataifa (Kiarabu, Kichina, Kiingereza, Kifaransa, Kirusi na Kihispania), Tamasha la Wikimania litatoa utafsiri mubashara kwa namna ya kuzunguka kwenda Kihindi, Kiindonesia, Kijapani, Kireno, Kireno cha Brazili, Kiswahili, Kituruki, na Kiukreni. Lugha hizi zilichaguliwa kulingana na idadi ya wazungumzaji ulimwenguni (ikiwemo iwapo kama lugha fulani ni lugha ya wengi kikanda), ukubwa wa idadi ya jamii za wahariri hai , kiasi cha washirika waliomo, na majibu ya utafiti wa Wikimania 2022. Wakati tungependa kusaidia utafsiri kwa lugha zote kwenye jumuiya zetu, tunatazamia kuendelea na kufanyia utafiti njia hii ili kuwezesha ushiriki mubashara katika lugha nyingi zaidi kuliko hapo awali.

Sehemu za ratiba zinazozunguka, ili kuwezesha muda mwafaka kwa kila mtu 

Programu za mtandaoni za Wikimania 2022 zita kidhi mahitaji ya washiriki kutoka maeneo yote ya saa. Lengo ni kukuza hali ya eneo husika kuangaziwa katika siku hiyo, pia wakati huohuo kupanga muda ambao utafaa kwa maeneo tofauti tofauti. Tulitaka kupanga kwa kuzingatia muktadha wa dunia nzima, kutengeneza ratiba ambayo inaenda kwa masaa mengi ili kuruhusu mwingiliano baina ya kila kanda na kila kanda nyingine.

Siku ya 1 itafunguliwa ikiwa na sehemu moja ya ratiba itakayofanyika masaa ya baada ya kazi kwa ukanda wa Asia-Oceania, na pia inaingiliana na maeneo mengine, kuruhusu watu kutoka maeneo mbalimbali kuwa sehemu ya kuanza kwa tamasha. Siku ya 2 itakuwa na maeneo mawili katika ratiba, wakati wa mchana na wakati wa jioni kwa Latin America, ikitenganishwa na Hackathon. Siku ya 3 itakuwa na maeneo mawili katika ratiba pia, wakati wa mchana na wakati wa jioni kwa Ulaya, ikitenganishwa na Hackathon. Siku ya Kimataifa itakuwa na programu zitakazotenganishwa na sherehe zitakazofanyika ulimwenguni kote. Siku ya 3 na ya 4 zitatumia vizuri fursa ya kufanyika mwishoni mwa wiki na nyongeza ya Lisaa limoja la programu za Wikimania. Kwa kila siku, sehemu ya kufahamiana itapatikana kwa masaa kadhaa baada ya programu.

Siku ya 1 – Asia – Oceania
Agosti 11
Siku ya 2 – Marekani Kuanzia Agosti 12Siku ya 3 – Ulaya, Afrika, Mashariki ya KatiAgosti13Siku ya 4 – Global DayAgosti 14
Masaa ya ProgramuWikimania: 9:00 UTC – 15:00 UTCWikimania: 14:00 – 16:00 UTC
Hackathon: 16:00 – 22:00 UTCWikimania: 22:00 – 2:00 UTC
Wikimania: 7:00 – 12:00 UTC
Hackathon: 12:00 – 17:00 UTC
Wikimania:17:00 – 20:00 UTC
Wikimania: 8:00 – 12:00 UTCSherehe mbalimbali ulimwenguni: 12:00-15:00 UTC
Wikimania: 15:00 – 19:00 UTC
Utafsiri Mubashara kwa lugha kuu Kiarabu, Kichina, Kifaransa, Kihispania, KirusiKiarabu, Kichina, Kifaransa, Kihispania, KirusiKiarabu, Kichina, Kifaransa, Kihispania, KirusiKiarabu, Kichina, Kifaransa, Kihispania, Kirusi
Utafsiri Mubashara kwa lugha za nyongezaKihindi, Kiindonesia, KijapaniKibrazili KirenoKiswahili, Kituruki, KiukreniKihindi, Kiindonesia, Kijapani, Kibrazili Kireno, Kiswahili, Kituruki, Kiukreni
Wazungumzaji wanaweza kuzungumza katika lugha yoyote kati ya hizo na kupokea tafsiri mubashara kwenda Kiingereza, na wazungumzaji watakaokuwa wakiwasilisha kwa kiingereza watapata tafsiri mubashara kwenda lugha hizo zote. 

Matukio mahalia ya ana kwa ana

Kama sehemu ya Wikimania mseto, Washirika wa Wikimedia kutoka ulimwenguni watakuwa wakiandaa matukio ya ana kwa ana yenye namna ya mwingiliano, kutoka sherehe za kutazama Wikimania hadi warsha za kuhariri, mpaka sherehe za kulala usingizi na mandari. Matukio mengi ya hivi yatakuwa wazi kwa jumuiya pana kimtandao. Matukio haya ya ana kwa ana yanaweza kujichomeka moja kwa moja kwenye tukio la mtandaoni, au kutoa masaa ya ziada ya programu au hata pengine usaidizi kwa lugha za nyongeza. Taarifa kuhusiana na matukio haya zitachapishwa kama sehemu ya programu kwa wiki zijazo.

Upo tayari kushiriki?

Usajili utafunguliwa hivi karibuni, hivyo kaa chonjo!

Tufuatilie hapa kwenye Diff au kwenye Twitter, Instagram, au Facebook  kwa masasisho ya karibuni.

No comments

Comments are closed automatically after 21 days.