Kichwa: Behind The Screen barani Africa

Matokeo ya harakati za Wikimedia barani Africa ni kubwa na dhahiri!

Behind the screen barani Afrika ni sehemu ya mfululizo mpana zaidi unaoadhimisha Wanawikimedia wasiochoka ambao hufanya maarifa ya bure yaonekane. Inaleta hadithi za ‘scrini’ kutoka Afrika kwa lengo sahili  la kushirikisha, kuheshimu na kusherekea matokeo. 

Mfululizo pia unalenga kupeleka mbele Mpango wa Mwaka wa Wikimedia Foundation wa 2022-23 na lengo la mkakati wa harakati la Usawa wa Maarifa. Mpango wa kila mwaka unazungumzia juu ya Kuendeleza Usawa wa Maarifa kupitia Mwelekeo Madhubuti wa Kikanda na mfululizo huu unaadhimisha matokeo ya kikanda hasa.

Moja ya hadithi kubwa ya matokeo chanya kutoka Afrika, ambayo inaenea katika bara kubwa ni ukuzaji wa ujuzi na uongozi. Hili ni eneo ambalo harakati barani Afrika zimepiga hatua kubwa. 

Jamii nyingi barani Afrika ziliipa kipaumbele Ukuzaji wa ujuzi na uongozi, ambayo ni mojawapo ya mapendekezo 9 ya mkakati wa harakati, wakati wa majadiliano ya kuweka kipaumbele kwa Mkakati wa Harakati mwaka 2019. Behind the Screen barani Afrika , inaadhimisha matokeo yaliyotokana na harakati katika kanda hiyo na  wakati huo huo ikikuza umuhimu wa maeneo haya husika kwa jamii katika eneo hilo.

Kulingana na Bobby Shabangu, ambaye ni rais wa sasa wa Wikimedia Afrika Kusini, ukuzaji wa ujuzi na uongozi ni muhimu sana kwa jamii za Kiafrika “kwa sababu zinahakikisha kwamba ujuzi sahihi unatolewa kwa wanawikimedia wapya, ambayo inahakikisha ukuaji na uendelevu wa harakati.

Kama Euphemia Uwadu, Mwanzilishi Mwenza wa Wiki Vibrance anavyosema, “Vijana wanajiunga na harakati na kupata ujuzi mkubwa.” Ujuzi huu unaanzia kwa utawala, uandaaji, mawasiliano na uongozi na kuvuka mpaka kwa jamii zinazoibuka na zilizoimarika katika eneo hili.

Ronald Romeo, Jamii ya Wikimedia Sudan Kusini anasema “kwa kuzingatia kwamba sisi ni jamii mpya, imekuwa muhimu sana kwetu kuongozwa juu ya hatua za kuchukua na binafsi inanipa ujasiri mkubwa kujua kwamba siko peke yangu.”


Tazama video kamili kuona Behind The Screen ya Afrika!

Manukuu yanapatikana kwa Kifaransa na Kiswahili