Wikipedia hakika haiwezi kutenganishwa na maisha ya Johnny Au. Mhariri huyu wa Wikipedia ya Kiingereza amekuwa akihariri kila siku tangu Novemba 11, 2007, jambo linalomfanya kuwa Mwanawikipedia mwenye mwendelezo mrefu zaidi wa kuhariri. Mwezi huu tunasherehekea kazi yake nzuri na majitoleo yake ya muda mrefu na yanayoendelea kwaajili ya maarifa ya bure.
Johnny Au alianza kuchangia kwenye Wikipedia mnamo mwaka 2006, na ikafika mahala fulani uhariri ukawa sehemu ya maisha yake ya kila siku. Nina tabia ya kuhariri kila siku. Mimi huwa nahariri ninapoamka na ninahariri kabla ya kwenda kulala ili kuhakikisha kwamba ninadumisha mwendelezo wangu wa kuhariri, anasema.
Kila siku Johnny huangalia orodha yake pana ya maangalizi, ambayo inajumuisha makala zinazohusiana na mji wake pendwa wa Toronto. Kuanzia timu za michezo za nyumbani na maghala ya sanaa, hadi mfumo wa usafiri wa Toronto – Johnny ni mkereketwa wa mambo yote yanayohusiana na Toronto, na kwa umakini hutazama kwa makini makala za Wikipedia zinazouhusu mji huo mkuu. Ikiwa ni pamoja na makala ile anayoipenda zaidi: makala kuhusu Sanaa za Umma za Toronto zilizopo kwenye njia ya chini ya ardhi kwa sababu hakika anafurahia sana kutazama kazi za sanaa za umma zilizopo kwenye mfumo wa treni ya chini ya ardhi.
Yeye hujikita zaidi katika kufanya mahariri madogomadogo ya matengenezo: kusahihisha tahajia na lugha, kurekebisha uharibifu, kuongeza picha na kusahihisha makosa. Aina hii ya kazi ya bila kuchoka, ya kina, ya kila siku ni muhimu kwa kutunza ubora wa Wikipedia. Na haijasahaulika: Majitoleo ya Johnny katika kudumisha makala ya timu ya besiboli ya Toronto Blue Jays dhidi ya uharibifu ilipelekea kuvivutia baadhi ya vyombo vya habari na kupelekea kuandikwa kwa makala kuhusu nyota huyu wa Toronto.
Tabia ya kuhariri kila siku na upendo thabiti kwa Wikipedia, na ukereketwa wa maarifa ya bure, ndio humfanya aendelee kuhariri. Siku baada ya siku, kwa miaka 15 (na zaidi). Yeye hufanya takribani mabadiliko 10 kila siku, ambayo yanaleta jumla ya kuvutia ya mabadiliko 64,000 katika Wikipedia ya Kiingereza. Na zaidi ya siku 5700 za uhariri endelevu.
Mwendelezo huu wa uhariri wa Johnny haukuwa unakosa vitisho na changamoto wakati huo wote. Ilitokea karibia na kipindi kile cha mayowe ya kusitisha intaneti kwa muda mfupi katika historia ya Wikipedia, kuzima kwa intaneti mwaka 2012. Kutokana na maamuzi ya wanajumuiya wa Wikipedia, ambao walipinga sheria iliyoonekana kuwa na madhara katika kazi zao, Wikipedia ya Kiingereza haikupatikana kwa saa 24 – sio tu kwa kusoma, lakini pia hata kwa kuhariri. Kwa bahati nzuri, tofauti za saa za eneo zilimsaidia Johnny kudumisha mwendelezo wake wa kuhariri. Kuzimwa kwa intaneti kulianza usiku wa manane kwa mfumo wa Saa za kawaida za Mashariki, huku mwendelezo wa mahariri ya Johnny ukizingatia mfumo wa saa wa UTC. Tofauti ya masaa matano kati ya hiyo mifumo miwili ilimpa mhariri wetu wa kila siku nafasi ya kufanya uhariri wake wa kila siku hata baada ya hayo yote.
Wakati Toronto inasalia kuwa mada inayopendwa zaidi ya uhariri wa Johnny Au, sio jambo pekee kati ya anayoyapenda sana. Kama Mwanawikimedia wa kweli, Johnny ana uwanda wa mambo mengi anayoyapenda: yeye ni mpiga kinanda, mpenda sayansi, mtu anayevutiwa na isimu, upigaji ramani, usafiri wa umma, astronomia na michezo. Pia anaendeleza shauku ya sanaa ya kidijitali na upigaji picha wa majengo na majengo mengine huko Toronto yanayoendelea kujengwa.
Angependa ulimwengu ujue miradi ya Wikimedia ni ya kutegemewa zaidi kuliko tovuti nyinginezo nyingi, licha ya kuwa miradi ya Wikimedia huzalishwa na watumiaji. Kuna watu wengi ambao hawaiamini miradi ya Wikimedia kwa sababu za kiitikadi (hasa wakati wa janga la COVID-19 na Uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2020), wanapendelea tovuti ghushi za kubofya zilizojaa habari uongo na upotoshaji. Ni changamoto kubwa kuwashawishi wengine kwamba miradi ya Wikimedia haina upendeleo wa kiitikadi, anasema. Wakati huo huo, ustahimilivu wa jamii kwa habari potofu mbele ya hili janga na maandalizi kabla ya chaguzi zenye utata vimethibitisha kuwa na ustahimilivu katika ulimwengu wetu.
Alipoulizwa kuhusu ushauri anaowapa wahariri wengine, anasema: Usikate tamaa kamwe. Pigana vita vizuri. Lazima tupigane dhidi ya habari za uongo na upotoshaji.
Asante kwa kazi yako Johnny na tunakutakia miaka 100 (na zaidi) ya uhariri wa kila siku!
Can you help us translate this article?
In order for this article to reach as many people as possible we would like your help. Can you translate this article to get the message out?
Start translation