Sio siri kwamba wakutubi huleta Wanawikimedia wazuri. Iwe ni kwa sababu ya shauku ya pamoja ya maarifa au nguvu kuu katika kufanya kazi na vyanzo, hifadhidata na kategoria, au ukweli rahisi kwamba wakutubi ni wanadamu wa kipekee, tunajua kwamba wanastawi katika miradi ya Wikimedia. Na kama unahitaji mfano kamili wa mfanyakazi wa maktaba, ambaye pia ni Mwanawikimedia wa kipekee, chukua mfano wa Alice Kibombo. Yeye ni mchangiaji wa Wikipedia, Wikidata, Wikisource, na Kikundi cha Watumiaji cha Jumuiya ya Wikimedia Uganda. Kuanzia mwanzo mnyenyekevu akiwa kama msomaji wa Wikipedia hadi jukumu la kuleta mabadiliko kama mwalimu na msaidizi wa jamii, Alice Kibombo amekuwa mtu wa kusisimua katika harakati za kufikia maarifa ya binadamu bila vikwazo. Na leo tunasherehekea kazi yake.
Alice, mkutubi huko Goethe-Zentrum Kampala, alianza safari yake ya Wikimedia mwaka 2017. Bado anajifunza kila siku, lakini alichojua kwa hakika ni kwamba hili lilikuwa jambo ambalo hangechoka kufanya. Kuchangia Wikimedia kumebadilisha jinsi anavyouona ulimwengu na kuwashirikisha hadithi na watu wengine. Alice alisema kwamba ‘Hii inaweza kuonekana kama ni ubinafsi lakini mwanzoni niliingia kwenye jukwaa hili ili kuchangia mada ambazo hazikuwa na makala lakini zenye maslahi kwangu – hili halijabadilika”.
Kazi hii ya kutunza kumbukumbu inaweza kushuhudiwa katika miradi ya Wikimedia. Alice anashiriki kikamilifu katika Wikipedia ya Kiingereza, ambapo aliongeza zaidi ya makala 70, nyingi kati ya hizo kuhusu wanasiasa wa kike wa Uganda na kushiriki katika kampeni inayopendwa na wasimamizi wa maktaba: #1lib1ref, ambayo inawaalika wakutubi duniani kuongeza nukuu kwenye Wikipedia. Pia anahariri Wikidata na Wikisource, ambazo zote zinajumuisha hadi zaidi ya mabadiliko 9000 katika miradi ya Wikimedia.
“Miradi ya Wikimedia inaonekana kuingiliana na inafurahisha sana kujua kila mmoja una nini katika huduma ya ufikiaji wa bure bila kizuizi kwenye jumla ya maarifa ya mwanadamu,” Alice anasema.
Wikimedia ni zaidi ya kuhariri kwa mtazamo wake Alice. Yeye ni mfanyakazi wa kujitolea katika Jumuiya ya Watumiaji wa Wikimedia ya Uganda, shirika lenye wasifu tofauti wa kampeni zilizopangwa, miradi ya elimu na ushiriki katika harakati za kimataifa za Wikimedia.
Alice pia ana uzoefu kama Mwanawikimedia mkazi katika shirika la African Library and Information Associations (AfLIA). Jukumu hilo la mwisho lilikuwa badiliko kubwa kwake: “Baada ya uzoefu huu, maisha yangu ya kikazi hayajawahi kuwa sawa tena. Ninajivunia zaidi watu ambao nimekutana nao njiani na mabadiliko wanayoyaongoza katika jamii zao,” anasema.
Kwa hivyo wakati Alice anaweza kuwa alianza safari peke yake sasa ni sehemu ya familia ya Wanawikimedia wenzake sio tu nchini Uganda bali ulimwenguni kote. “Kushiriki katika harakati za Wikimedia kumenipa jukumu la kuwa mchangiaji anayewajibika zaidi, mtu ambaye ni rasilimali kwa jamii na vile vile mwalimu.”
Tunashukuru kwa kuwa na wewe katika harakati, Alice!
Can you help us translate this article?
In order for this article to reach as many people as possible we would like your help. Can you translate this article to get the message out?
Start translation