Nilizungumza nanyi nyote hapo nyuma mnamo mwezi wa Novemba kuhusu swali ninaloamini kuwa ndilo swali muhimu zaidi linalozikabili harakati za Wikimedia: je, tutahakikishaje kwamba Wikipedia na miradi yote ya Wikimedia inakuwa ni ya vizazi vingi vya watu? Ningependa kumshukuru kila mtu ambaye alichukua muda kulitafakari swali hilo na kunijibu moja kwa moja, na sasa kwa kuwa nimepata nafasi ya kutumia muda kutafakari majibu yenu, nitawashirikisheni nilichojifunza.
Kwanza, hakuna sababu moja ya watu wanaojitolea kuchangia. Ili kukuza vizazi vingi vya watu wa kujitolea, tunahitaji kuelewa vyema sababu nyingi za watu kuchangia wakati wao kwenye miradi yetu. Kisha, tunahitaji kuangazia kile kinachotutofautisha: uwezo wetu wa kuchangia maudhui ya kuaminika huku taarifa potofu na upotoshaji zikienea kwenye intaneti na kwenye mifumo inayoshindana ili vizazi vipya vivutiwe. Hii ni pamoja na kuhakikisha tunafanikisha dhamira ya kukusanya na kuwasilisha jumla ya maarifa yote ya binadamu kwa ulimwengu kwa kupanua wigo wetu wa taarifa zinazokosekana, ambazo zinaweza kusababishwa na ukosefu wa usawa, ubaguzi au upendeleo. Maudhui yetu yanahitaji pia kutumika na kubaki kuwa muhimu katika mabadiliko ya intaneti yanayoendeshwa na akili bandia na uzoefu tele. Mwisho tunahitaji kutafuta njia za kufadhili harakati zetu kuwa uendelevu kwa kujenga mkakati wa pamoja wa bidhaa na mapato yetu ili tuweze kufadhili kazi hii kwa muda mrefu.
Mawazo haya yataonekana katika mpango wa kila mwaka wa Shirika la Wikimedia wa 2024-2025, sehemu ya kwanza ambayo ninawashirikisheni ninyi leo katika mfumo wa rasimu ya malengo ya kazi yetu ya bidhaa na teknolojia. Kama ilivyokuwa mwaka jana, mpango wetu wote wa kila mwaka utazingatia mahitaji ya teknolojia ya hadhira na mifumo yetu, na tungependa kusikia maoni yako ili kujua kama tunaangazia matatizo yanayofaa. Malengo haya yanatokana na mawazo ambayo tumekuwa tukisikia kutoka kwa wanajamii kwa muda wa miezi kadhaa iliyopita kupitia Mazungumzo:2024, kwenye orodha za wanaopokea barua pepe na kurasa za mazungumzo, na katika matukio ya jumuiya kuhusu bidhaa na mkakati wa teknolojia kwa mwaka ujao. Unaweza kuona orodha kamili ya malengo ya rasimu kwenye Meta-Wiki.
“Lengo” ni mwelekeo wa kiwango cha juu ambao utaunda miradi ya bidhaa na teknolojia tunayochukua kwa mwaka ujao wa fedha. Malengo haya ni mapana kwa makusudi, yanawakilisha mwelekeo wa mkakati wetu na, muhimu zaidi, ni changamoto zipi tunazopendekeza kuzipa kipaumbele kati ya maeneo mengi yanayoweza kuangaziwa kwa mwaka ujao. Tunawashirikisheni hili sasa ili wanajamii waweze kusaidia kuunda mawazo yetu ya mapema na kabla ya bajeti na malengo yanayoweza kupimika kutekelezwa kwa mwaka.
Maoni
Sehemu moja ambayo tungependa kusikia maoni haswa ni kuhusu kazi yetu iliyopangwa chini ya jina “Matukio ya Wiki.” “Matukio ya Wiki” inahusu jinsi tunavyowasilisha, kuboresha, na kuvumbua kwa ufanisi jinsi watu wanavyotumia Wiki moja kwa moja, iwe kama wachangiaji, watumiaji au wafadhili. Hii inahusisha kazi ya kusaidia teknolojia na uwezo wetu mkuu na kuhakikisha kuwa tunaweza kuboresha matumizi ya wahariri wanaojitolea – hasa, wahariri walio na haki nyingi – kupitia vipengele na zana bora zaidi, huduma za tafsiri na uboreshaji wa mifumo.
Haya hapa chini ni baadhi ya maswali ya tafakari kutoka kwenye mijadala yetu ya hivi majuzi ya kupanga, na baadhi ya maswali kwa ajili yenu nyote ili kutusaidia kuboresha mawazo yetu:
- Kujitolea kwenye miradi ya Wikimedia kunapaswa kuhisiwa kuwa ni kitu chenye kutoa motisha. Pia tunafikiri kwamba uzoefu wa ushirikiano wa mtandaoni unapaswa kuwa sehemu kuu ya kinachowafanya wajitoleaji warudi. Je, tunapaswa kuwafanyia nini wanaojitolea kupata manufaa ya uhariri, na kufanya kazi vizuri zaidi ili kuunda maudhui ya kuaminika?
- Uaminifu wa maudhui yetu ni sehemu ya mchango wa kipekee wa Wikimedia kwa ulimwengu, na kinachowafanya watu kuja kwenye jukwaa letu na kutumia maudhui yetu. Tunaweza kuunda nini kitakachosaidia kukuza maudhui ya kuaminika kwa haraka zaidi, lakini bado kiwe ndani ya ulinzi wa ubora uliowekwa na jumuiya kwenye kila mradi?
- Ili kusalia kuwa muhimu na kushindana na mifumo mingine mikubwa ya mtandaoni, Wikimedia inahitaji kizazi kipya cha watumiaji ili kuhisi kuwa wameunganishwa kwenye maudhui yetu. Je, tunawezaje kurahisisha maudhui yetu kugundulika kiurahisi na kuingiliana nayo kwa wasomaji na wafadhili?
- Katika enzi hizi ambapo matumizi mabaya ya mtandaoni yanashamiri, tunahitaji kuhakikisha kuwa jumuiya zetu, mifumo na mfumo wa huduma vinalindwa. Pia tunakabiliwa na kubadilika kwa majukumu ya utiifu, ambapo watunga sera wa kimataifa wanatazamia kuchagiza faragha, utambulisho, na kushirikisha habari mtandaoni. Je, ni maboresho gani ya uwezo wetu wa kupigana na unyanyasaji yatatusaidia kushughulikia changamoto hizi?
- MediaWiki, jukwaa la programu na violesura vinavyoruhusu Wikipedia kufanya kazi, inahitaji usaidizi unaoendelea kwa muongo mmoja ujao ili kutoa uundaji, udhibiti, uhifadhi, ugunduzi, na utumiaji wa maudhui wazi ya lugha nyingi kwa kiwango. Ni maamuzi gani na uboreshaji wa jukwaa tunaweza kufanya mwaka huu ili kuhakikisha kuwa MediaWiki ni endelevu?
Can you help us translate this article?
In order for this article to reach as many people as possible we would like your help. Can you translate this article to get the message out?
Start translation