Kujenga Ulimwengu Bora, Picha Moja na Kuhariri kwa Wakati Mmoja: Kuadhimisha Brahim Faraji

Translate this post

Leo tunamsherehekea Brahim Faraji, mfanyakazi wa kujitolea wa Wikimedia wa muda mrefu, ambaye anahakikisha kuwa Wikimedia Commons imejaa picha zenye ubora wa hali ya juu!

Mnamo 2016, utaftaji wa Brahim Faraji wa kutafuta njia ya kuleta matokeo chanya ulimpeleka kwenye Harakati za Wikimedia. Akiwa anavinjari mtandaoni, Wikipedia ilivutia macho yake. Punde si punde aligundua kuwa ilikuwa ni zaidi ya ensaiklopidia: “Nilitafuta kujua zaidi kuhusu Wikipedia, jinsi inavyofanya kazi na historia yake, kisha nikapata taarifa kuhusu harakati za Wikimedia na maadili yake ambayo yalinisukuma kufanya kazi kwa bidii zaidi na kwa ari”, anasema.

Farajiibrahim, CC BY-SA 4.0 , via Wikimedia Commons

Sehemu yake ya kuingilia ilikuwa ni Wiki Loves Monuments, shindano la kimataifa la picha ambalo huwahimiza washiriki kunasa picha za maeneo ya urithi wa kitamaduni kote ulimwenguni. Wazo la kuhifadhi historia kupitia picha lilimvutia sana Brahim. Mnamo mwaka wa 2016, alipakia picha kwenye shindano hilo kwa mara ya kwanza, huku picha zake nne zikiwa katika nafasi ya kumi bora za Makumbusho ya Morocco katika mashindano hayo ya Wiki Loves Monuments! Tangu wakati huo, amekuwa mpiga picha anayejitolea kwenye Wikimedia, akichangia picha kwenye mada mbalimbali: kutoka Tamasha la TBOURIDA (hina kwenye harusi ya Morocco), hadi kifaa cha kimuziki kiitwacho rebabu, kutoka anga ya kushangaza yenye dhoruba hadi maeneo ya urithi wa kitamaduni ya Moroko. Kazi yake imekuwa sehemu ya kampeni za picha za Wikimedia kama vile Wiki Loves Africa, Wiki Loves Folklore na hasa Wiki Loves Monuments, ambapo Brahim alipata hadhi ya kuwa mwanafainali kwa miaka minne mfululizo.

Brahim pia aligundua mradi mwingine ambao ni Wikimedia:education. Alijiunga na programu ya Kusoma Wikipedia Darasani na kuwa mmoja wa wakufunzi wa kwanza kuthibitishwa. Hiyo ilikuwa mnamo 2020, wakati shule zilipotatizika na janga la Corona na zilipokuwa zikitoa elimu kwa njia ya mtandao. Licha ya changamoto hizo, Brahim alianzisha miradi ya elimu ya Wikimedia nchini Morocco, huku akifuata ndoto ya kuwa na ulimwengu bora, ambayo anaielezea: “pamoja na vizazi vyote vilivyokuzwa na ujuzi unaohitajika kuelewa jinsi vyombo vya habari vinavyotolewa, kufikia na kutathmini maudhui mtandaoni na kutambua upendeleo na mapungufu ya kiujuzi katika taarifa zinazotumiwa.”

Hivi karibuni Brahim akawa mwanachama wa harakati za kimataifa, akishiriki katika matukio mbalimbali ya kimataifa, kama vile Wiki Arabia au Wiki Indaba (akiwa thabiti katika roho yake kuwa mpiga picha alipiga picha nyakati za jumuiya ya Wikimedia!).

Majitoleo makubwa kwa misheni ya Wikimedia kunachochea shauku ya Brahim. Alipoulizwa kuhusu motisha yake, alisema “Maadili ya harakati na moyo wa ushirikiano. Ninahisi kuwa sehemu ya familia ya ulimwenguni wote, inayoishi ili kufanya ulimwengu kuwa mahali pazuri kupitia maarifa ya bure.”

Brahim anatambua kwamba bado kuna mengi ya kufanikisha. Anaona kwamba bado hakuna ujuzi wa kutosha kuhusu Wikimedia, kitu ambacho kinaweza kusababisha idadi ndogo ya watu kujiunga na harakati zetu. Lakini yeye ni mtu mwenye matumaini kiasili: “Hakuna kilicho rahisi lakini kila kitu kinawezekana! Kwa hivyo, Usikate tamaa, thamani yako ya ziada ya kuifanya dunia kuwa mahali pazuri ina thamani kubwa sana!”, anawashauri Wanawikimedia wenzake.

Asante kwa michango yako yote, Brahim na kwa kuhifadhi maarifa kuhusu urithi kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Can you help us translate this article?

In order for this article to reach as many people as possible we would like your help. Can you translate this article to get the message out?

No comments

Comments are closed automatically after 21 days.