Kamati ya Uendeshaji ya Wikimania inakaribisha vikundi vya jumuiya na ushirikiano wa kikanda kuwasilisha maombi ya kutaka kuandaa Wikimania 2027 na 2028. Kamati pia iko tayari kwa majadiliano na wale ambao wana mawazo ya matoleo ya Wikimania baada ya 2028. Wikimania ni mkutano wa kimataifa wa kila mwaka ambao huleta pamoja wanachama wa harakati za Wikimedia, kukuza ushirikiano, kujifunza, na kusherehekea maarifa huria.
Kwanini uandae Wikimania?
Kuandaa Wikimania kunaipa jumuiya yako fursa ya kipekee ya kushirikisha eneo na kukuza ushirikiano huku ikichangia katika harakati za kimataifa za Wikimedia. Ni nafasi ya kuwaleta watu pamoja katika mazingira ya kushirikisha, na kuangazia matokeo ya miradi ya Wikimedia duniani kote.
Tunakaribisha makundi ya jumuiya ambayo yana shauku na uwezo wa kusimamia majukumu ya ugavi na utaratibu wa kuandaa mkutano huu mkubwa kwa ushirikiano na shirika la Wikimedia Foundation. Ikiwa ungependa kuandaa Wikimania ya mwaka 2027 au 2028, tungependa kusikia kutoka kwako – unaweza kueleza nia yako kwenye wiki au tutumie barua pepe kwa wikimania@wikimedia.org. Mwito wa Kuonyesha Nia utasalia wazi kuanzia tarehe 2 Desemba 2024 hadi 27 Januari saa 23.59 popote duniani.
Kamati ya Uendeshaji ya Wikimania
Kamati ya Uendeshaji ya Wikimania ndiyo msimamizi wa mkusanyiko mkubwa zaidi wa kimataifa wa harakati za Wikimedia. Tunahakikisha tukio linabaki kuongozwa na kulenga jumuiya. Wengi wetu ni waandaaji wa zamani wa Wikimania au wahudhuriaji waliobobea, na tuna shauku kuhusu kile tunachoweza fanikisha tunapokutana pamoja.
Can you help us translate this article?
In order for this article to reach as many people as possible we would like your help. Can you translate this article to get the message out?
Start translation